Zijue sifa 8 za nyumba iliyopambwa vizuri na kuleta furaha .... via


 via


 
via
 via
via
via

Kuna sifa 8 ambazo nyumba iliyopambwa vizuri ni vizuri iwe nazo.Sifa hizo ni kama ifuatavyo:
 1. Rangi:
Rangi mbalimbali huleta mvuto ndani ya nyumba zikipangiliwa vizuri,mfano katika picha hizi unaona meza ya pink, kabati la njano,mito,ukuta uliochorwa n.k
2. Maua
Maua fresh  hupendeza ndani ya nyumba na kuleta harufu nzuri.
3. Picha
Picha za familia,ndugu jamaa na marafiki na hata picha  za kuchora zinakumbusha wanafamilia matukio mbalimbali katika familia, mfano picha hapo juu zimewekwa ukuta mzima.
4. Mpangilio mzuri
Mpangilio mzuri wa fanicha ,vyombo, kwa kila kitu kuwa na mahali pake huifanya nyumba kuwa na mpangilio na hivyo hewa kuzunguka vizuri,na kuraisisha kila mwanafamilia kurudisha kila kitu mahali pake.
5. Usafi
Nyumba iliyosafishwa vizuri sakafu,paa ,kuta nje na ndani na kuondoa mavumbi hufanya nyumba yoyote kupendeza.
6. Vitabu
Nyumba ni vizuri iwe na vitabu mbalimbali kwa ajili  ya wanafamilia kujisomea na kuongeza maarifa katika mambo mbalimbali.
7. Michezo
Michezo kama chess,puzzles,karata,scrabble,checkers  n.k ni mizuri kwa familia kuwa nayo kujiburudisha na pia watoto katika familia watajifunza.Michezo ya namna hii ni mizuri kukuza akili na kumbukumbu.
8.Muziki:
Muziki wa taratibu (sio wakati wote)kwa kipindi fulani .Wakati mwingine ni vizuri kuwa na ukimya kutuliza akili.

 Sifa hizi kwa pamoja huifanya familia kuyafurahia makao yake na kama tunavyofahamu mahali pazuri na pasafi ni muhimu kwa afya ya familia.Hivyo pamba nyumba yako ni vizuri kwa familia yako.

No comments:

Post a Comment

1