Vitu vizuri... ni kwa ajili ya nani?

source and here

Vitu vizuri , maua mazuri, maeneno mazuri ya kuvutia kama (hiyo picha ya tatu juu),chakula kizuri na kilicho na mvuto,vitu vya zamani kama hayo masanduku,vitu vilivyotengenezwa kwa mikono kama hicho kikapu, usafi wa nyumba ni vitu ambavyo vinaleta nyongeza ya furaha katika maisha yetu ya kila siku. Hivyo ni muhimu kuvipa umuhimu wake ,kuvitunza na kujifunza zaidi jinsi ya  kuvijumuisha katika maisha yetu ya kila siku.Kwa mfano ukipakua chakula kwanini usijiwekee kwenye sahani nzuri wewe mwenyewe kuliko kuweka tu sahani nzuri kabatini eti za wageni?.

No comments:

Post a Comment

1