( Henri Mattise; woman with hat)
images via pinterest
Jinsi gani unaweza kuanzisha biashara kwa kusoma blog hii?
Jibu: Kwa kuwa msomaji wa kudumu wa sophie's blog utaweza kuanzisha biashara ya upambaji wa maofisi , majumbani n.k .
Jinsi ya kuanza fuata hatua hizi:
1. Chagua jina la biashara yako.
2. Tengeneza portifolio (kielelezo cha kazi ulizoisha fanya)
(a)Kwa kuwa ndipo unaanza pamba nyumbani kwako harafu piga picha pia omba upambe kwa ndugu, jamaa na rafiki,nyumbani au ofisini harafu piga picha nzuri za jinsi ulivyopamba.
(b) Ziweke kwenye album hizi ndizo utakazo waonyesha wateja wako ili waone kazi yako. (c) Baada ya kupata wateja kumbuka kila unapopamba upige picha hiki ndicho kielelezo cha kazi nzuri unayoifanya.Ni jinsi hii hata ma designer wakubwa wanafanya.
3. Tengeneza business cards. 4. Toa matangazo sehemu mbalimbali ili watu wajue unatoa huduma hiyo.
5. Tembelea blog hii mara kwa mara na blog yangu nyingine absolutelyawesomethings.com upate idea mbalimbali.
Ni muhimu kuhakikisha picha zako ni nzuri.
6. Kama utakuwa na swali au nyongeza weka kwenye comments.
7. Unaweza.
Ushauri mzuri huu na rahisi kueleweka. Safi sana.
ReplyDeleteAsante sana,nafurahi kusikia hivyo.
ReplyDeleteasante sana, naiwaza sana hii biashara. Nafikiria kujifunza kudesign mapazia. Nadhan ntapata ujuzi mwingine humu
ReplyDelete