Wapenzi wa SophiesClub...nitarudi karibuni.

In memory of my Sweet Brother,Tunakupenda sana.

japokuwa kifo ni mwisho wa maisha ya duniani lakini sio mwisho wa uhusiano.
Nakupenda sana Kaka yangu.

Wapenzi wa Sophies Club,sijawasahau.Nimejipa likizo kuomboleza msiba wa Kaka yangu mpenzi (Baba Emma) uliotokea miezi miwili iliyopita.Imebidi nijipe likizo ndefu ili nikusanye nguvu,nitarudi karibuni kujumuika nanyi. Wakati huo nakuomba burudika na blog ya Mpwa wangu Emma, hapa. Asanteni sana kwa kutembelea SC .Enjoy,tenda wema na mpende jirani yako maisha ni mafupi.Karibu tena na tena.

7 comments:

 1. Ahsante kwa taarifa dadangu. Pole sana tena sana naona tupo kwenye maombelezo hayo wengi kwa kweli mwenzio nami ninaombeleza mdogo wangu pia. Sisi tuliwapenda lakini Mungu anawapenda zaidi. Tuzidi kuwaombea. Pole sana kwani najua ni hali gani unayo Namwomba Mungu azidi kukupa nguvu pia familia yote.Amina

  ReplyDelete
 2. Dua njema ya kumrehemu kaka yetu mpenzi!

  ReplyDelete
 3. Wapenzi Yasinta na Emu-three nawashukuru sana sana kwa maneno yenu ya faraja na maombi yenu. Asanteni sana.Yasinta pole na wewe kwa msiba wa mdogo wetu Mungu azidi kukupa nguvu na faraja na familia nzima, nitakukumbuka katika sala. Nawashukuru sana.

  ReplyDelete
 4. Pole sana. Mungu awapeni nguvu katika kipindi hiki kigumu na amweke marehemu katika raha ya milele. Amina.

  ReplyDelete
 5. Sophie Tupo pamoja nawe pia pole sala nami ntakukumbuka katika sala Marehemu wote wastarehe kwa amani!!

  ReplyDelete
 6. pole sana mpenzi Mungu ailzE Roho ya Marehemu mahala Pema Peponi AMIN

  ReplyDelete
 7. Prof. Mbele na Mariam asante sana kwa maneno yenu ya faraja.Mbarikiwe wote.

  ReplyDelete

1