Vitabu,maua na rangi...Images courtesy of elleinterior
Shelf ya vitabu,maua mazuri mbalimbali na rangi za kuvutia kama hiyo njano ni mpangilio mzuri hufanya sehemu ivutie na ionekane imetulia.Pia sakafu ya rangi utakayoichagua inapendeza.Muhimu ni kuwa mbunifu na pia kuweka vitu vinakupendezea wewe,vinavyoelimisha au vinavyokukumbusha matukio mbalimbali katika familia yako.Enjoy!

2 comments:

  1. Nimefurahi kuona mada hii ya kupanga vitabu nyumbani. Nina vitabu vingi kule Tanzania na hapa nilipo sasa; vinazidi elfu tatu.

    Bado naendelea kununua vitabu. Ni uhai na afya ya akili na pia ni raha yangu.

    Kama sitaweza kujenga nyumba maalum ikawa maktaba, itabidi nitafute mkakati wa kuviweka katika nyumba nitakayokuwa nakaa, na kujaribu kuvitafutia mpango mzuri wa kupendeza kama ilivyo katika ukurasa wako huu.

    ReplyDelete
  2. Asante Prof.,kwa kweli vitabu ni muhimu sana mie huwa nasema ni kama tochi maana inakuangazia mambo mengi mwenyewe bila kumsumbua mtu. Ni vizuri na muhimu sana kujisomea na kuwa na vitabu

    ReplyDelete

1