Ramani na watoto

Images via desiretoinspire
Kupamba ni pamoja na kuweka vitu ambavyo vitawaelimisha wanaoishi sehemu husika,kwa mfano ramani kubwa ukutani sio tu inaelimisha bali inapendezesha. Vilevile picha mbali mbali au kufunikia kitambaa kizuri kwenye canvas ni sanaa inayojitosheleza. Watoto wetu nao tusiwasahau,kuwawekea rangi za kuvutia na kuwapangia vizuri na kuwawekea sehemu yao ya kujisomea (picha ya 4 kutoka juu) ni muhimu . Namna hii si tu unawafundisha kuwa wasafi,kuwa na mpangilio na kuwa kujisomea ni muhimu bali pia unawapa ujumbe  pia  unawapa mwelekezo wa vitendo ambao ni muhimu katika maisha yao baadaye.Enjoy!

3 comments:

  1. Ahsante sana dada Sophie nimwefurahia pia nimejifunza kitu.

    ReplyDelete
  2. Na mimi nimeipenda hii! Ahsante sana.

    ReplyDelete
  3. Jamani asanteni kwa kuacha maoni,nafurahi kuwa mmeipenda na kujifunza kitu.Karibuni tena

    ReplyDelete

1