Maua ndani ya nyumba....kama hivi

Images courtesy country living

Ukichuma japo ua moja na kuweka ndani ya nyumba ni kitu kizuri. Jiulize kwanini huwa tunawapelekea wagonjwa maua?au mtu anahitimu tunampa maua au kwenye misiba tunapamba maua au mtu akijifungua au watu tuwapendao tunawapa maua, ni kwasababu maua ni kiungo cha upendo. Basi ni vizuri tukipamba maua ndani ya nyumba zetu.Utasema sina chombo kizuri special kwa maua,usipate taabu, tumia chupa (kama picha hapo juu) au tumia kopo tupu unaweza kulipakaa rangi kama( picha ya tatu kutoka juu inavyoonyesha ). Weka maua mengi tu kama picha ya juu kabisa inavyoonyesha utajikia kama umekaa bustanini. Ni vitu vidogo kama hivi ambavyo huongeza furaha mahali unapoishi. Jaribu na Enjoy!

No comments:

Post a Comment

1