Kupamba vizuri kwa ubunifu na bei poa...
I Images courtesy of country living
Nani asiyependa kupata kitu kizuri kwa bei rahisi?! Namna hii hata katika mapambo unaweza ukapamba kwa bei poa kabisa na kufurahia matokeo maana unapata mapambo ya kipekee na ya kufurahisha maana umetengeza mwenyewe. Kwa mfano picha ya juu kabisa ni box limewekewa frame ya picha kwa juu,picha ya pili toka juu kabati limepigwa rangi nyeupe kufananisha na kiti (harafu rangi ya fanicha ikielekeana na rangi ya ukuta huifanya sehemu kuoneka kubwa faida nyingine hiyo). Picha ya tatu viti 3 vimewekewa ubao wa moja kwa moja na hivyo kuwa bench,na ya picha ya nne unakusanya candle holders za aina mbalimbali na kugundisha kwenye tray na kuwa na mkusanyiko wa aina yake.Kupamba vizuri ni kuwa mbunifu kama ilivyo katika kazi nyingine.Haya tutumie picha au tupe tip ya ubunifu wako.Enjoy!

No comments:

Post a Comment

1