
Hummus tayari kwa kulia mkate au chapati

Image courtesy of all-creatures
Rafiki yangu aliniomba niwe nablog mapishi maana huwa anapenda kujaribu vyakula mbalimbali kuona watu wengine wanapendelea nini. kama alivyo rafiki yangu hata mie hupenda kujaribu kupika vyakula toka nchi mbalimbali. Nitakuwa napost mapishi toka nchi mbalimbali ninayoyapenda tofauti na yale tuliyoyazoea kwetu.
Hummus ni mchanganyiko wa chickpeas na vikolombwezo mbalimbali kama unavyoona hapo chini(nimejaribu kutafuta kiswahili cha chickpeas bila mafanikio naomba kama unajua tafadhali tuachie jina,kwenye kamusi online wanaita njegele lakini hizi sio njegele). Ni Chakula kinacholiwa sana na watu wa Mashariki ya kati hasa Waisrael. Huwa napenda kutengeneza kwakulia mkate ua chapati.
Mahitaji (kuhusu kiasi huwa nakisia tu maana unataka mchanganyiko uwe kama uji mzito,hapa nitajaribu kuweka makisio ila utaangalia jinsi unavyopenda)
Chickpeas -huwa natumia kopo 1
Limau -nusu
Kitunguu swaumu- kipande kimoja
Pilipili manga-saga punje kama kumi,kama imesagwa-robokijiko cha chai
Maji -robo kikombe
Chumvi-kidogo tu
Olive oil-kijiko kimoja kikubwa
Cumin-nusu kijiko cha chai
Kitunguu maji kidogo -robo
Parsel (nafikiri inaitwa giligilani)-(Ukipenda) kidogo kwa kupendezesha kama hapo kwenye picha.
Jinsi ya kutengeneza;
Changanya Chickpeas,kitunguu swaumu,kitunguu maji na blend kwenye blender mpaka imesagika .Ongeza maji,olive oil,chumvi,pilipilimanga na maji ya limau blend tena.
Toa na weka kwenye sahani tayari kwa kulia mkate au chapati. Enjoy
chickpeas zinaitwa dengu au adesi tanzania tunatumia kama mboga au kupikia bajia, ni chakula kikuu cha wahindi.
ReplyDeletechick peas kwa kiswahili ni "DENGU".
ReplyDelete