
nephytis

spider plant

dwarf date palm

sword fern

Maua nyumbani au ofisini sio mapambo tu bali ni mazuri kwa afya yako kwani husafisha hewa na kufanya mazingira yako ya nyumbani au ofisini kupendeza kufanyia kazi au kuishi.Kwa hiyo wewe kama sio mpenzi sana wa kupamba basi pata ua (au yote) kati ya hayo juu japo kwa nia ya kuboresha hewa ya nyumbani kwako au ofisini. Kama una watoto wadogo au wanyama kama paka au mbwa ni muhimu kuhakikisha hawachezei maana maua mengine yanaweza yakawadhuru wakiyala. Pia kuna maua zaidi yafanyayo kazi hii majina yake hapa na hapa ila haya nimeona ni post haya maana yanapatika kirahisi kwetu na utunzaji wake sio mgumu. Tuzipende afya zetu na sehemu tunazoishi,Enjoy!
Ukiwa na maua ya ndani ni muhimu kuyatoa nje ili yapate mwanga wa jua hasa mida ya asubuhi kuelekea mchana (kabla jua halijawa kali sana), ni muhimu kujua kila aina ya ua lako linahitaji kutolewa nje kila baada ya siku ngapi na kwa masaa mangapi
ReplyDeleteBennet asante kwa tip itatusaidi wengi,hii hata mie nitaanza kufanya hivi
ReplyDelete