Utambaje chumba cha watoto?

Image courtesy best decorating ideas


Image courtesy of rice
Image via mikodesigns
Image via frilliedesigns

Images courtesy of rice

Tusiwasahau watoto wetu maana wakilala vizuri na kukaa pazuri ndio inavyotakiwa. Ukiwawekea mazingira mazuri itawavutia hata kuweka chumba chao katika mpangilio ymfano kuchukua kitu na kukirudisha mahali pake ili wasihangaike wakiihitaji tena. Rangi za kuvutia na kabati lenge draws ndio siri kubwa ya kupamba chumba cha watoto. Vitu hivi unaweza ukatengeneza mwenyewe bila hata gharama kubwa kwa mfano 1.hili bedcover,unatengeneza kwa kuunganisha vipande vidogo vidogo vya vipambaa mbalimbali (kama utapenda kujua jinsi gani acha comment nitablog hiyo pia).2.Pia unaweza kufuma foronya kwa mtindo wa krosia au tengeneza kutokana na kanga,vitenge au vitambaa vya maua. 3. Kitu kingine ni kuweka wallpapers kama ya 4 au kuchora ukutani mchoro watakao upenda wao. 4. Kingine ni kutumia vikapu kuwekea vitu vyao mbalimbali unaweza ukaweka jina kwenye kila kikapu. 5. Tumia mapazia ya maua.
Vitu vingine vya muhimu kuwekea ni pamoja meza au shelf ya kuwekea vitabu na madaftari yao. na saa ya ukutani maana itawasaidia kujua muda.
2 comments:

  1. Nimependa hii na nadhani nitajitahidi kuwatengenea wanangu vyumba vyao yaani kufanya mabadiliko. Asante kwa tip.

    ReplyDelete
  2. Asante kushukuru Yasinta, nafurahi kusikia hivyo.

    ReplyDelete

1