Somo linazidi kueleweka TZ...angalia upambaji HomezDeco na Ladyjaydee

Image via homezDeco

Leo nimefurahi kuona blogs mbili wanapromote upambaji na umuhimu wa kuyapenda mazingira yako,somo linazidi kueleweka! Blogs hizo ni homezDeco na ladyjaydee. Nimefurahi kwa kuwa naona wengi tunaanza kuona umuhimu wa kuyapenda mazingira yetu ( kupitia maoni yaliyotolewa). Kwa msisitizo zaidi kama ambavyo huwa nasisitiza ktk blog posts zilizopita, sehemu unayoishi iwe ni nyumba yako au nyumba /chumba cha kupanga ni mahali pako kwa wakati huo na ni reflection yako, ni vema na ni ustaarabu ukipapanga vizuri na kupapendezesha ndani na nje.Sio lazima vitu/mapambo viwe vya gharama bali chagua ulivyo na uwezo navyo na vingine una-recycle na kutengeneza mwenyewe kama ambavyo nimekuwa niblog .Sio tu patakuongezea ufanisi maana kila kitu unajua kilipo bali pia patakupunguzia stress. Tuyapende mazingira yetu kama tunavyojipenda!

No comments:

Post a Comment

1