Uzuri wetu wa asili tumeupotezea wapi?vipodozi na madhara yake

Image via fashionmanifesto
Mwanamitindo Alek WekImage via photobucketMisuko ya nywele za nyuzi
Image via charcoalink
Mwimbaji Jill Scott na afro la nywele zake
image via fanpics

Uzuri wetu wa asili tumeupotezea wapi?
Sijui tulaumu watengenezaji wa vipodozi vya karne hii au tujilaumu wenyewe kwa kupoteza uzuri wetu wa asili.Aina nyingi za urembo wa karne hii unahatarisha afya zetu ( na za watoto tumboni iwapo mama mjamzito anatumia vipodozi hivi) na pia unatupotezea uzuri wetu wa asili mfano mzuri ni vipodozi vya ngozi na dawa za nywele. Nimekuwa nikifikiri mtu ukimuuliza hivi nywele zako za asili zinafananaje nahisi wengi tumesahau maana tunaweka dawa juu kwa juu. Kuna aina nyingi za kupendeza kama unataka kubadili staili suka mitindo mbalimbali kwa muda mfupi mfupi mradi upumzishe nywele zako kutokana na madhara ya unayoweza kupata kwa kutumia hizi dawa kwa muda mrefu. Sasa basi kabla hujanunua hivi vipodozi vya ngozi,makeups n.k kwa usalama wa afya yako tembelea cosmeticdatabase website ambayo itakuonyesha ni kwa kiasi gani vipodozi hivyo vina madhara. Hizi picha hapo juu nimezipenda sana nikaona nizipost kwakuwa zinawaonyesha hawa akina dada wanavyothamini uzuri wao wa asili.Na kama unavyowaona bado ni wa "kileo" na wenye maendeleo vile vile.Tumia vipodozi vya asili,jali,thamini na jivunie ngozi na nywele zako za asili, ijali afya yako utapendeza zaidi na kujiamini na kwa mtindo huu utakuwa umeyajali mazingira maana vipodozi vya chemikali hatima yake uharibu mazingira.Enjoy

3 comments:

 1. Mara nyingi nimesema ninaringa kwa kuwa mTanzania naringia ngozi yangu laini, machocho yangu meupe na nywele zangu nyeusi. Ahsante sana kwa hii mada ni kweli watu tunahangaika mno kutafuta uzuri wakati uzuri tunao. Mimi bado kabisa sijaelewa na nadhani sitaelewa kabisa.Kwa nini mtu anakataa uasili wake? kazi kwelikweli.

  ReplyDelete
 2. Wazungu walipofika Afrika na kulibatiza bara letu kuwa la giza, na sisi wenyewe kuwa tusiostaarabika, kwamba eti tulikuwa tunaishi kama wanyama tu bila "elimu" wala maarifa yoyote - wakatuletea hii elimu ya "kisasa" na Yesu wa Nazareti, walifanikiwa mno kutupondaponda kisaikolojia. Baada ya miongo kadhaa ya uhuru, kupondwapondwa kwetu huku kunaendelea kujidhihirisha zaidi na leo hii tunaiga kila kitu cha kizungu na kudharau kila kitu kilicho chetu. Tunaionea aibu ngozi nyeusi na tunajibidisha sana kuachana nayo kwa kutumia makemikali makali ambayo wakati mwingine yanaishia kuleta saratani za ngozi na matatizo mengineyo ya kiafya - isa tu eti mtu awe mweupe. Huwa nasikitika sana nikimwona binti aliyejaliwa ngozi nyeusi nyororo ya Kiafrika halisi akiwa amejibabuababua - huku fanta, huko kokakola na huwa najiuliza kwa nini?

  Suala hili limeshalalamikiwa sana na watu wengi na pengine kulalamika na kusema tu hakutoshi. Pengine inabidi tuliingize katika mitaala ya historia na masomo mengineyo shuleni tuwafundishe vijana wetu kujivunia Uafrika wao. Sasa tumefikia hatua hata lugha zetu za kiasili zimekuwa ni lugha za kuonewa aibu kwani ni lugha za kishamba - kila mtu anataka kuongea lugha za Kizungu. Na serikali inavyoonekana imekisikia kilio hiki ndiyo maana inajipanga sawasawa kukiondoa Kiswahili kutoka shule za msingi. Sijui tunakoelekea lakini siyo kuzuri. Wakoloni kweli walituweza na Steve Biko alikuwa sahihi kabisa aliposema "The most potent weapon in the hands of the oppressor is the mind of the oppressed" They still own our minds!

  ReplyDelete
 3. Kwakweli msemayo ni kweli kabisa tunahitaji kuelimika katika suala hili. Mradi hizi blog zimekuja juu katika masuala mbalimbali nahisi itasaidia .Asanteni na karibuni tena na tena na tena

  ReplyDelete

1