Bluu,zambarau,kijani na wall papers
Images courtesy of skonahem
Natumaini wasomaji wangu nyote wazima kwetu salama!Nimeona upambaji toka Skonahem ( natamani ningejua kusoma lugha yao) wanamapambo mazuri. Picha hizi nimeipenda zaidi kwakuwa nilitaka kuongelea jinsi ambavyo wall papers zinavyopendezesha nyumba/chumba hasa zikiwa ni rangi za kutulia kama bluu,kijani,zambarau. Ila usiweke wallpapers aina moja nyumba nzima zitakuchosha. Weka aina tofauti tofauti vyumba utavyochagua na zenye maua madogo madogo au majani kama hapo juu maana huwa hazichoshi kuziangalia.Enjoy na karibu tena!

3 comments:

  1. Da Sophie ulikuwa umepotea karibu tena. Hilo gazeti la shonahem ni gazeti ambalo sikosi kulinunua kila likitoka ni kweli lina mapambo mazuri sana ni kiswid. Kwa hiyo mi nafaidi dada:-)

    ReplyDelete
  2. Asante Yasinta,niliona nijipe kijilikizo kifupi.Kweli unafaidi maana nimelipenda,ila nimefurahi kujua unasoma kiswid basi nikiona kingine nachokipenda nitakuomba unitafsirie.hii ndio faida nyingine ya watu kuishi kila mahali wote tunapata uhondo. Karibu tena

    ReplyDelete
  3. Sawa Ntafurahi kuwa msaada kwako. nafurahi kupita hapa na kuona kazi yako nzuri idees nk.

    ReplyDelete

1