Sanaa ya krosia (crochet) - Brazil na Marekani


Images courtesy elainecroche
Sanaa ya krosia imekua sana nchini Brazil wakina mama wanajipatia kipato kwa kufuma vitu mbalimbali. Japo kwetu watu wengi wanaijua sanaa hii tumekuwa hatuikuzi sana na wengi kuishia kufuma vitambaa na sweta za watoto kidogo kidogo. Hatujachelewa kazi kama hizi za mikono zinasoko sana sehemu mbalimbali duniani. Dada huyu wa elainecroche amefuma mkoba mfano wa huo alionao Mwanadada Halle,unaona alivyoufuma vizuri kwa ufundi na kwenye website yake anaonyesha video mbalimbali za kazi zake kama utapenda kujifunza na hapo hapo anauza video hizo na kujiongezea kipato. Ijaribu sanaa hii ni nzuri.Enjoy!

2 comments:

  1. Nimevutiwa na kijiji hiki pia nimejifunza mengi ambayo nilikuwa siyafahamu hapo awali.
    Hongera sana mdau

    ReplyDelete

1