Rangi zilizopoa...tusiziogope.!Images courtesy of bhg
Njia ya haraka ya kupamba nyumba/chumba na kubadili sura yake ni kupaka rangi.Ukitaka chumba kionekane kikubwa zaidi chagua rangi iliyopoa.Rangi mf. kijani (kibichi) na bluu (maji ya Bahari) zimepoa na kawaida rangi zilizopoa huleta mwanga zaidi na huwa hazichoshi hivyo kukutuliza. Mazoea yetu katika nyumba nyingi huwa ni kupaka rangi nyeupe,yenyewe hupendeza pia.Jipe changamoto, wakati ujao pamba kwa kupaka rangi kama hizo hapo juu zinapendeza na zimetulia. Usisahau kuchagua rangi zilizo nzuri kwa afya na kwa mazingira yaani zisizo na kemikali za Lead.Furahia mazingira mazuri!

No comments:

Post a Comment

1