Upambaji magari...nani kasema akina kaka/baba sio wapambaji wazuri?Image courtesy of pingmag

Upambaji ni popote pale hauna mipaka na si kazi ya wajinsia moja tu kama kwetu watu wengi wanavyochukulia.Waendesha magari makubwa huko Japan wanapenda kupamba magari yao kama picha zinavyoonyesha hapo juu kama zilivyotolewa na ping magazine. Natamani wamiliki wa daladala Tz wangeanza kuzipamba ndani kwa matangazo ya biashara,namna hii wasafiri tungefurahia mazingira ya kuvutia na wakati huo huo kupata habari kuliko tu kuweka miziki mikubwa ambayo wakati mwingine inafunguliwa kwa sauti ya juu sana mpaka watu wote hamsikilizani.Pia hii ni njia ya kujipatia kipato zaidi na pia ajira kwa watengenezao matangazo na mapambo mbalimbali.3 comments:

  1. niliona video ya hawa wapambaji wa magari Japan, ni kama walevi wa mapambo, yaani wanavyopenda magari yao ni sawa na vile mama anavyompenda mwanae - addiction kabisa na huwa wanashindana! - ajira tena!

    ReplyDelete
  2. sophie gari kama hizi nyingi sana hapa japan, na wengi wao wanao pamba gari namna hii ni hobby tu si gari za kufanyia kazi, kama unaweza kumuona mtu anapenda lorry basi si la kazi ni la hobby ndipo utakuta gari ndani inaengenezewa kila kitu kama nyumba, pia kuna sehemu wenye magari kama haya huwa wanakutana kila mtu anaangali gari la mwenzie lilivyo pambwa, pia gharama za upambaji mwengine ni kubwa kuliko gharama ya gari

    ReplyDelete
  3. Inafurahisha kuona jinsi watu tulivyo na hobby mbalimbali,mswahili aliyajua mapema akasema tembea uone!

    ReplyDelete

1