Umetimiza ndoto ya nani?Tafakari

Image courtesy of Oprah.com

Prof. Mbele ameandika kuhusu mchango wa wabeba mabox,nimependa maoni hayo na comments zilizotolewa na wasomaji . Moja ya maoni ni kuwa wabeba mabox wanatoa mchango kwa pato la taifa na kuanzisha miradi mbalimbali.Pia nafikiri kwa kutoa ajira na kuwa na miradi mbalimbali kuboresha maisha namna hii wanafanya ndoto zao na za watu mbalimbali zitimie.Hii kwa ujumla imekumbusha habari hii kutoka oprah.com ambapo Oprah na rafiki yake Gayle wamemtimizia kijana huyu ndoto yake .Vile vile habari ya kijana huyu Bernard LaChance inaonyesha umuhimu wa kuwa na determination, umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii,kufikiri , kuwa creative na kuwa na plan A, B na C kutimiza unachotaka kukifanya. Itakufundisha na kukufurahisha na kukufanya ufikiri na labda siku moja utamtimizia mtu mmoja ndoto yake.Isome hapa.

2 comments:

  1. Wow!! Niliwahi kuandika kuhusu tofauti ama ulipo mstari kati ya ndoto na ufunuo. Naamini kuna wakati TUNAFUNULIWA lakini twauona ufunuo kama ndoto na ndio maana hatufanyii kazi.
    ASANTE kwa makala njema

    ReplyDelete
  2. Shukrani kwa kutupanua mawazo na hizi taarifa. Hatimaye, uwezekano upo kuwa wale wasiojiamini au wasiojithamini kwa kazi wafanyazo watabadili fikra na kuwa na mwelekeo unaofaa.

    ReplyDelete

1