Mapambo na vitu vya zamani...viko wapi?
Images courtesy of decorativecountryliving.

Amini usiamini hili ni duka,linapendeza eh! ni duka website yake ni decorativecountryliving .Wanauza mapambo na vitu mbalimbali vya zamani na vipya. Huwa najiuliza hatima ya vitu vya zamani kule kwetu sipati jibu,kwa mawazo yangu nafikiri asilimia kubwa inaishia kutupwa kinyume na nchi nyingine nyingi ambapo wanathamani sana vitu vyao vya zamani na wanavitumia kwa mapambo,kuweka historia na pia katika sanaa mbalimbali.Maduka kama hili ni mifano mizuri ya kuiga ambapo watu wangepata sehemu ya kuuza vitu vya zamani na vitu hivi vingethaminika zaidi.Pia ni njia ya kuweka historia na kutunza mazingira na wakati huu tukipamba na kupendezesha tunapoishi.Kama unajua mfano wa duka kama hili TZ usisite kutuelekeza,tutashukuru.Enjoy!

No comments:

Post a Comment

1