Kwao kila sanaa ni muhimu ,kwetu je?


Image courtesy of Institute for figuring

Institute For Figuring inamaonyesho ya coral reef (matumbawe nafikiri ndio kiswahili chake) zilizoshonwa kwa sanaa ya krosia (crochet).Inaonyesha pia sanaa ya krosia kwa kutumia taka za plastic.Kama mmoja wapo wa wakereketwa katika suala zima la kuhifadhi mazingira nimependa mpango huu maana unaelimisha umuhimu wa kutunza mazingira kwa kutumia sanaa. Namna hii inafikisha ujumbe kwa mvuto wa uzuri sanaa hii na hapo hapo kushirikisha jamii(crocheters) kwa kuonyesha ufundi wao katika fani hii vile vile kuweka kumbukumbu.

No comments:

Post a Comment

1