Kuwasomea watoto vitabu.

Image courtesy of teriandjack


Professor Mbele ameandika article nzuri sana kuhusu umuhimu na faida za kuwasomea watoto vitabu. Kwa kweli hata mie nafikiri tukianza tukijenga tabia ya kuwasomea watoto kila siku itawajenga sana. Mie na uzee wangu wote huu!bado nakumbuka Mama yangu alivyokuwa hakosi kutusimulia hadithi tena wakati mwingine akiwa anapika,na akipata nafasi anatutafsiria hadithi maana na vitabu vya kiingereza ambavyo hatukuwa tunavielewa.Bidii yake tunaiona maisha mwetu.Pia tukijisomea wenyewe tunajiendeleza na tunakuwa mfano bora kwa watoto,watoto wanajifunza zaidi kwa mifano.
Niliwahi kusoma mahali kuwa mtu inabidi ujitahidi kujua kitu kipya kila siku na njia rahisi ya kupata mafundisho mazuri nikujisomea . Isome article hiyo hapa na kitabu chake cha African and American: Embracing Cultural Difference ambacho na recommend kama unaweza kisome ni hiki. Japo sijakimaliza (nasoma kwa mwendo wa kinyonga mpaka nifike) ni kitabu kinachoelimisha na kuburudisha vile vile.

No comments:

Post a Comment

1