Ubao mzuri wa matangazo wa gunia.

Image courtesy of craftzine.com
Nimeona huu ubao wa matangazo (sijui hiki ndicho kiswahili chake sahihi?) uliotengenezwa kwa kufunika ubao kwa gunia kutoka craftzine.com nikaona niipost. Nchi za Magharibi wana tilia mkazo ku-recycle au re-use bidhaa mbalimbali na watu wanapenda sana kutumia bidhaa hizo.Mfano ni kama gunia hilo lilivyotumika na kwa uchunguzi wangu wa haraka haraka ofisi hii isingeshindwa kununua ubao special kama ile tuliyoizoea!. Nafikiri hata sisi tukithamini jitihada kama hizi si tu kwamba tutakuwa tunahifadhi mazingira bali tutaongeza ajira. Ukipenda kutengeneza Ubao huu angalia maelekezo yake toka craftzine .

2 comments:

  1. Asante Da Sophie. Kwa ujumla haya mengi yanaigwa ama kuonwa kwetu na kuendelezwa kwao. Lakini japo yanatoka kwetu bado hatuyathamini. Ni mengi ambayo yamekuwa yakitendeka kwetu kwa miaka lakini yakapuuzishwa akilini mwetu na sasa yakifanyika kwao twaona ni ustaarabu. Tuna uwezo mkubwa wa ku-recycle na hiyo ingetusaidia kuokoa mazingira na pesa nyingi sana ambazo zingeelekezwa kwingine kwenye uhitaji. Angalia magari kwenye vituo vya polisi na kwingine yanavyoozea pale na kuwa vyanzo vya magonjwa. Ona mataruma na "vichwa" vya treni kwenye stesheni zetu za matengenezo yanavyoozea mle. Angalia mifuko ya "rambo" mitaani inavyoharibu mazingira na kuhatarisha afya za wakazi. Ni mengi ambayo tungeweza kufanya. Watu huku wamefiki hatua ya ku-recycle hata maji taka ili kukabiliana na upungufu wa maji hasa ambayo ni kwa matumizi yasiyo ya kunywa kama viwadani, lakini nyumbani, licha ya kuwa na maji mengi, bado tuna shida kwa kuwa viwanda vyagombania maji ambayo yangeenda kwa wanywaji, na wao kutmia yaliyokuwa recycled kwa kuwa ni kwa wajili ya kupoza mitambo.
    Ni changamoto nzuri Dada na twashukuru kwa hili.
    Blessings

    ReplyDelete
  2. Mzee wa Changamoto asante sana. Yaani yote uliyoyasema ni kweli kabisa na kazi kubwa bado tunayo.Nafurahi atleast tumepata haya "majanvi" kama ulivyoyaita ili tubadilishane mawazo labda tutasogeasogea maana kama asemavyo mswahili haba na haba ujaza kibaba.Karibu tena comments zako are highly appreciated.

    ReplyDelete

1