Faida ya Rangi zinazowaka,
Image courtsy of bhg.com

Heri ya Sikukuu kwenu wote!
Nimekuwa naufikiria sana usemi niliousikia kwenye interview moja kwamba "bright colors are therapeutic" Naamini ni kweli rangi zinazowaka (bright colors) zinafaida fulani kwetu kiafya.Sijajua science inasemaje kuhusu hili itabidi nilifanyie kazi kidogo au msomaji kama unajua ukweli katika hili tutashukuru ukituelimisha. Nimeweka picha hizi tatu kutoka bhg.com ili ufanye jaribio, hebu fikiria umeshinda unafanya kazi katika nyumba hizi 3 asubuhi mpaka jioni. Je unafikiri utakuwa katika same mood kwenye nyumba zote tatu au la?
Si vibaya ukijaribu kuweka mapambo, furniture, accessories za rangi mbalimbali nyumbani au ofisini kwako naamini utayafurahia mazingira yako zaidi na vile vile utakuwa unadumisha upambaji.

1 comment:

  1. Nadhani sasa nitakuwa mpambaji mzuri kwa kupitia humu. Kupamba ni sanaa na naona ina wenyewe kama wewe. Kazi nzuri dada.

    ReplyDelete

1