Ufunguzi

Image courtesy of karibu-stenger.net


Mpendwa msomaji nachukua nafasi hii kukukaribisha sana katika hii blog yangu na wewe sophiasclub.blogspot.com. Kwanza kabla ya yote nilitaka hasa kuiita sophie's club ila nikakuta jina hili limeisha chukuliwa wajanja wameniwahi!Lakini nitaendelea kutumia nick name kama watu wengi wanvyoniita sophie hivyo usije ukashangaa na kufikiri ni mtu mwingine. Nakukaribisha sana . Nimeamua kuanzisha blog ya pili (ya kwanza ni http://absolutelyawesomethings.blogspot.com/) kwa sababu ninataka tuwe na uwanja wa kutuunganisha na kuongelea mambo mengine na especially yanayohusu maisha,afya,kazi,biashara na uwekezaji,mazingira,malezi.
Lengo hasa la blog hii ni kuelimisha, kuburudisha, kupeana mawazo,ubunifu ,kujengana,kuelekezana,kuwekeza na mengine mengi hivyo karibu sana na kumbuka mchango wako ni muhimu sana tafadhali .Na zaidi kumbuka kuuliza si ujinga hivyo kama unaswali lolote tafadhali uliza. Cha mwisho naomba tujalibu kutumia lugha nzuri ili mwisho wa siku blog hii iwe kiunganishi chetu wote.
Mara kwa mara tutakuwa tukiwakaribisha watu wenye uzoefu katika nyanja mbalimbali watupe majibu mbali mbali na pia kutakuwa na fursa ya watu kutoa mawazo na kuchangia. Karibu sana

2 comments:

 1. Hello Sophie,
  Asante sana kwa kazi kubwa unayoifanya,nashindwa kuelewa unapata wapi muda wa kumuangalia mtoto na kutafuta vitu kama hivi!
  Mawazo uliyotoa ni mazuri tu,tutafute topic na kuzijadili. Najua utakuja na mawazo kemkem,manake nakuaminia mwanangu!!
  haya ngoja niandike kidogo leo manake ni mara ya kwanza,mambo mengi yanakuja mbeleni.
  Farida

  ReplyDelete
 2. asante mpendwa,Kusema ukweli muda hautoshi ila nautafuta mpaka naupata dakika 15 tu zinanitosha maana mambo ya kuandika ni mengi. Haya leta mawazo mapya uwanjani and keep checking!

  ReplyDelete

1